Mtayarishaji filamu wa michael matthews anafarijika beyonce kutambua filamu yake iliyompa motisha katika utunzi wa albamu ya cowboy carter

Mtayarishaji filamu wa Afrika Kusini Michael Matthews anasema anafarijika kuwa Beyonce alitambua filamu yake ilimpa motisha katika utunzi wa nyimbo katika albamu yake mpya ya Cowboy Carter.

Wiki iliyopita, mwimbaji huyo wa Marekani alifichua kwamba kila wimbo kwenye albamu hiyo ulipata msukumo kutoka kwa filamu tofauti ya nchi za Magharibi, na kwamba mara nyingi alikuwa akionyesha filamu hizo kwa nyuma wakati akirekodi.

Moja ya filamu alizozitaja ni Fingers For Marseilles, filamu ya kisasa ya Western 2017 iliyoongozwa na Matthews, na filamu ya kwanza ya Magharibi ya Afrika Kusini.

"Ni heshima kubwa kutambuliwa na msanii shupavu na mbunifu kama Beyoncé," Matthews aliliambia gazeti la Afrika Kusini The Sowetan.

"Na kujumuishwa miongoni mwa watengenezaji filamu kama vile [Quentin] Tarantino na [Martin] Scorsese," aliendelea, akiashiria filamu kama The Hateful Eight ya Tarantino na Scorcese ya Killers of the Flower Moon iliyoshinda tuzo ya Oscar, ambayo Beyoncé pia alitaja miongoni mwa ushawishi wa Cowboy Carter.

Matthews aliongeza kuwa ilikuwa muhimu kwa Beyoncé kutambua filamu ya Afrika Kusini.










Share: