Msanii davido wa nigeria achunguzwa kuhusu madai ya vitisho dhidi ya tiwa

Mwanamuziki nyota wa Afrobeats Davido anachunguzwa na polisi wa Nigeria baada ya mwimbaji mwenzake Tiwa Savage kumripoti kwa madai ya kumdhulumu na kumtishia.

Mvutano kati ya wanamuziki hao wawili mashuhuri uliripotiwa kuanza mwezi uliopita baada ya Tiwa kusambaza picha yake na mama wa mtoto mmoja wa Davido kwenye posti yake kwenye Instagram.

Katika ripoti yake ya polisi iliyonukuliwa na vyombo kadhaa vya habari vya ndani, Tiwa anasema kwamba Davido alichukizwa na ujumbe huo, akiona kama dhihaka dhidi yake.

Anadai kuwa Davido alijibu kwa "kuzungumza maneno ya dharau, maovu " dhidi yake.

Tiwa pia anamshutumu Davido kwa kutuma watu kumuonya "kuwa mwangalifu huko Lagos", ambayo anaiona kama "kinyume cha maadili" na "tishio la moja kwa moja kwa haki zangu za maisha, faragha na utu".

Davido bado hajajibu tuhuma hizo, Nyota hao wawili pia wameacha kufuatana kwenye Instagram.

Share: