Mpishi mashuhuri failatu abdul-razak afutiwa rekodi ya kupika

Mpishi kutoka Ghana Failatu Abdul-Razak alitumia masaa 227 kupika bila kusimama mnamo Januari 2024, ili kuvunja rekodi ya lan Fisher lakini rekodi yake hii ilikataliwa na Guinness World Records

Jaribio hilo limekataliwa na GWR. Mratibu wa timu yake, Kafui Dey, alithibitisha kukataliwa kwake Jumapili, huku sababu ikiwa ni "ukiukwaji wa miongozo mikali iliyowekwa na Guinness World Records."

Msemaji wa GWR alikiri juhudi zake, akisema, "Tunampongeza Failatu kwa juhudi zake kubwa na jaribio hili la rekodi lilikataliwa kutokana na miongozo kuhusu muda wa mapumziko kutotimizwa."

Jaribio la Failatu lilizua shauku kubwa kote nchini Ghana na Afrika. Wanasiasa, ikiwa ni pamoja na Makamu wa Rais Mahamudu Bawumia na watu mashuhuri walijitokeza kumuunga mkono Failatu katika kipindi chote cha mapishi.

Hii inamaanisha rekodi iliyowekwa na mpishi wa Ireland Alan Fisher bado inabaki palepale Fisher Alipika kwa saa 119 na dakika 57, zaidi ya saa 24 zaidi ya rekodi ya awali iliyokuwa ikishikiliwa na mpishi wa Nigeria, Hilda Baci.

Share: