Mistari ya thuger kutotumika kama ushahidi mahakamani

Inasemekana kuwa waendesha mashtaka waliwasilisha seti 17 za mashairi, wakisema kuwa maneno hayo "si mazuri,"

Timu ya wanasheria ya rapa Young Thug, imekuwa ikifanya kazi kwa bidii ili kuhakikisha kuwa mashairi ya nyimbo zake hayawezi kutumika kama ushahidi katika kesi yake inayomkabili,

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi Jumatano, jaji aliamua kwamba waendesha mashtaka wanaweza "kwa masharti" kutumia mashairi ya young Thug kama ushahidi.

Inasemekana kuwa waendesha mashtaka waliwasilisha seti 17 za mashairi, wakisema kuwa maneno hayo "si mazuri," na yanaweza kuthibitisha kuwa YSL ni genge.

Mwendesha mashtaka Mike Carlson alisema, "Heshima yako, mtu anaweza kuangalia shtaka hilo na kusema jambo moja ni la hakika, hiyo sio ndoto, watu wamekufa na kuuawa na kuna genge” Kesi ya Thug inatarajiwa kuendelea Novemba 27

Share: