Miss world 2024 krystyna pyszkova anajivunia mradi alioufanya nchini tanzania

Miss Czech, Krystyna Pyszkova ambaye ameshinda Taji la Miss World 2024 katika shindano lililofanyika Mumbai, India, Machi 9, 2024 anajivunia Mradi alioufanya Nchini Tanzania kwa kujenga Shule Mkoani Arusha. 

Kupitia kipengele cha ‘Beauty with Purpose’ ambacho kwa miaka ya hivi karibuni kimekuwa kikizingatiwa kwa wanaoshinda taji, Krystyna amesema alishiriki katika ujenzi wa Shule ya Mkondo wa Kingereza iitwayo Tanzania English School kwa Watoto Wasiojiweza kwa lengo la kuboresha Maisha ya wahusika. 

Upande wa Miss Tanzania katika mashindano hayo, Halima Kopwe alifanikiwa kuingia kwenye Kundi la Washindani 40 Bora kati ya 112 walioshiriki. 

Share: