Ndani ya studios za St bongo kipindi pendwa cha tv , The Bantu amefunguka mambo chungu nzima tusio ya fahamu husani kuhusu shindano la miss world na vile uzuri na urembo unavyo weza kuleta tija kwa warembo na taifa kwa ujumla hususani Miss Tanzania.
Miss Tanzania ni mashindano ya urembo ya kitaifa nchini Tanzania, yanayoratibiwa na kampuni ya The Look Company. Lengo kuu la mashindano haya ni kuchagua mrembo atakayewakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa kama Miss World na Miss Universe.
Sasa hapa tuna story za Miss Tanzania 2022 ndani ya studio zeni, Halima Ahmad Kopwe ni mrembo kutoka Mtwara, Tanzania, aliyejizolea umaarufu kama mshindi wa taji la Miss Tanzania 2022. Alikabidhiwa taji hilo rasmi mnamo Mei 20, 2022, katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, akiwabwaga warembo 19 walioshiriki mashindano hayo .
Tazama interview yake kusikiliza mengi yalio jiri na tulio yapokea kutoka, Bila shaka 2025: Shindano la Miss Tanzania 2025 linatarajiwa kufanyika hivi karibuni.