
Marioo ameandika historia mpya baada ya video zake mbili, “Mvua” na “Ha Ha Ha,” kushika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye YouTube Trending Now – Tanzania. Hatua hii inathibitisha nguvu yake ya kisanii na mapokezi makubwa ya kazi zake mbili zilizotoka kwa kufuatana ndani ya muda mfupi.
Kwa lugha ya muziki, hiki ni kisa kinachosimulia ubunifu na uwezo wa @marioo_tz kutoa nyimbo zinazopenya mioyoni mwa mashabiki kwa haraka, hasa mwanzoni mwa nusu ya pili ya mwaka 2025. Nyimbo hizo zimekuwa kubwa mitandaoni, zikitamba pia kwenye TikTok, moja ya majukwaa makubwa yanayokuza umaarufu wake.
Hii inaweza kuonekana kama njiapanda muhimu kwa CEO wa @badnationtz kuelekea hatua kubwa za kimataifa, kwani ameonyesha uwezo wa kutoa hits mfululizo bila kupoteza mvuto. Takribni miezi 7 iliyopita, albamu yake ‘#TheGodSon’ imechangia zaidi kuthibitisha ukuaji wa jina lake kama hitmaker asiye na mipaka, anayeheshimika na wasanii wenzake, vyombo vya habari na mashabiki.