Marioo amefunguliwa kesi ya madai ya tsh. 550,000,000 na kampuni ya kismaty kwa madai ya kuvunja mkataba

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Omary Mwanga "Marioo", amefunguliwa kesi ya madai na Kampuni ya Kismaty kwa madai ya kuvunja mkataba wa kutumbuiza kwa kutoonekana kwenye hafla ya Mr & Miss Vyuo Vikuu Kanda ya Kaskazini

Kulingana na madai yaliyowasilishwa Mahakama Kuu Masjala ya Wilaya ya Arusha mbele ya Jaji Joackim Tiganga imeelezwa Marioo na Meneja wake, Sweetbert Mwinula wanakabiliwa na tuhuma za kuvunja mkataba huo wa Septemba 23, 2021, wakidaiwa jumla ya Tsh. 550,000,000

Kesi hiyo inatarajiwa kusikilizwa Mahakama Kuu mnamo Machi 18 na 19, 2024

Share: