Marioo ameachia album yake yenye nyimbo 17 leo

Usiku wa leo Tarehe 29 November 2024 msanii wa bongofleva Omary Mwanga almaarufu kama Marioo aandika rekodi kwakuongeza album yake ya pili aliyoipa jina la The GodSon.


THEGODSON(TGS) itakua ni album yake ya pili kwani ya kwanza aliitoa tarehe 9 December 2022 na aliipa jina la The Kid You Know (TKYK).

The Godson imebeba kolabo 10 kati ya ngoma 17 zinazopatikana kwenye album hiyo na wasanii kama Alikiba, Harmonize, Aslay na wengine kibao ni miongoni mwa wanaokamilisha tracklist ya album hiyo.


Share: