Marekani: 50 cent ameshtakiwa kwa kumpiga mtangazaji na kipaza sauti

Rapa Mkongwe na Mfanyabiashara, Curtis Jackson a.k.a 50 Cent ameshtakiwa na Mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Power 106, Bryhana Monegain, anayedai jeraha alilopata baada ya kupigwa na Kipaza Sauti limeathiri mwonekano wake.

Ingawa tukio hilo linalodaiwa kutokea kwa bahati mbaya Agosti 2023, lilielezwa kusababishwa na kifaa hicho kumsumbua 50 Cent akiwa Stejini na hivyo kupata hasira na kuirusha pembeni ambapo kiliishia kumpiga Mtangazaji huyo usoni

Bryhana amedai anaendelea kuteseka kwa Msongo wa Mawazo juu ya tukio hilo na hivyo anataka kulipwa fidia za Mshahara aliopoteza wakati akiuguza jeraha, pamoja na gharama za matibabu na uharibifu mwingine.


Share: