Maafisa usalama (hsi) nchini marekani wafanya upekuzi kwenye nyumba za p diddy

Nyumba za Mfanyabiashara na Mwanamuziki Sean ‘Diddy’ Combs zilizopo Los Angeles na Miami zimevamiwa na Maafisa Usalama ikidaiwa wanafanya uchunguzi na upekuzi kuhusu tuhuma za Biashara ya Ngono na Biashara ya Binadamu zinazotajwa kuhusu staa huyo

Maafisa wa HSI ambacho ni Chombo Kikuu cha Uchunguzi cha Idara ya Usalama wa Taifa ya Marekani wamewafunga pingu baadhi ya Watu waliokutwa katika nyumba ya Los Angeles wakiwemo Watoto wa Diddy ambao ni King na Justin huku baba yao akiwa hajulikani alipo

Inadaiwa ndege Binafsi ya Diddy imeonekana ikielekea Visiwa vya Caribbean kwa mujibu wa Tovuti ya Flight Tracking Data

Share: