Leo imetimia miaka 11 tangu kufariki kwa mwanamziki albert mangwea

Ngoma ya Speed 120 Albert Mangwea (RIP) ft Chidi Benz iliyotoka mwaka 2010 kuna line Ngwea amechana “Na hata nikifa leo pengo langu halina spea coz mi ndo mi na hatuwezi kuwa pea”.

Miaka mitatu baadaye May 28, 2013 kipaji hichi cha muziki kilizima na kufariki dunia huko nchini South Africa na leo imetimia miaka 11 ya kumbukumbu ya kifo chake.

Moja ya sifa zake enzi za uhai wake ni kuwa mbele ya muda, mkali wa freestyle, kuandika, flows, kuimba na kurap, mcheshi na uwezo wa ajabu katika muziki.

Mpaka leo bado hatujaona wa kuziba pengo lake kimuziki kama alivyotabiri kwenye Speed 120 licha ya miaka yote hiyo kupita tangu kufariki.

Share: