Ghana iko mikono salama kwa upande wa muziki kutokana na kazi kubwa ambayo inafanywa na wasanii wake kama Sarkodie KJ Spio na wasanii wengine kutokea huko Ghana.
Kwa sasa KJ Spio anafanya poa na kazi yake "JEALOUS" ambayo ameshirikisha Sarkodie, Lowick Essien pamoja na Ambre' na tayari wameshaachia Official Video ya wimbo huo.
Mpaka sasa kazi hiyo "Jealous" imepata watazamaji zaidi ya Laki sita (600k) kwenye YouTube channel ya KJ Spio ikiwa na wiki mbili tu tangu imetoka.
KJ Spio na Sarkodie wamekuwa na urafiki wa muda mrefu na kusaidia kwa kiasi kikubwa kwenye muziki na hii inakuwa ni kazi ya pili kwa wao kufanya pamoja kwani miezi kadhaa iliyopita alichia "Undress You" wakiwa wamemshirikisha Oxlade.
Unawezeka kuzitama kazi zote hizo kwenye YouTube channel ya KJ Spio kupitia link hii hapa