Kiasi hicho cha fedha, ambacho ni matokeo ya mapato ya muziki wa Michael Jackson katika kipindi cha miaka 15 tangu kifo chake
Katherine Jackson, mama mzazi wa aliyekuwa Mfalme wa muziki wa Pop duniani, Michael Jackson, amekabidhiwa kiasi cha zaidi ya Dola Milioni 55 (sawa na TZS Bilioni 141) kama sehemu ya mali ya mwanae tangu kifo chake mwaka 2009, kulingana na taarifa kutoka kwa wasimamizi wa mirathi.
Hii inafuatia mzozo wa muda mrefu kati ya Katherine na wasimamizi wa mirathi, ambapo mzazi huyo amekuwa akipigania kupata mgao unaostahili kutokana na mafanikio ya muziki wa mwanaye.
Kiasi hicho cha fedha, ambacho ni matokeo ya mapato ya muziki wa Michael Jackson katika kipindi cha miaka 15 tangu kifo chake, kimewasilishwa kwa Katherine baada ya jitihada za kisheria za kurekebisha mgawo wake.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na TMZ, hatua hii imekuja baada ya rufaa iliyowasilishwa na Katherine kutokuridhika na mgao wa awali wa pesa za mirathi ya mwanaye.
Katherine Jackson, ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 93, amekuwa mstari wa mbele katika kudumisha na kulinda urithi wa Michael Jackson, na kupitia hatua hii, inaonekana amefanikiwa kupata mgao unaostahili wa mafanikio ya muziki wa mwanae.