Kanye west baada ya kukerwa na swali aliloulizwa kuhusu mke wake ampatia mkataba ripota wa tmz

Rapa Kanye Amempora Simu Ripota Wa TMZ Baada Ya Kukerwa Na Swali Aliloulizwa Kama Anambania Mke Wake "Bianca Censori" Kwa Kumnyima Uhuru Wa Kufanya Maamuzi Binafsi, Kutumia Mitandao Ya Kijamii N.k

Tukio Hili Limetokea Leo Wakati Kanye Akiwa Njiani Kuelekea Kwenye Shughuli Ya (Charlie Wilson Walk Of Fame) Hollywood. "Nimekuja Kumuunga Mkono Charlie Wilson Halafu Unauliza Maswali Ya Kipuuzi"

Kanye Alitumia Zaidi Ya Dakika 3 Kumchana Ripota Huyo Ambapo Mwisho Wa Siku Amempa Shavu La Mkataba Na Kumwambia Atamlipa Mara Mbili Ya Mshahara Wake Wa TMZ.

"Mpatieni Mkataba! Nitakulipa Mara Ya Mbili Ya Kile TMZ Wanakulipa"

Mwaka Jana Pia Kanye West alionekana akimpora simu shabiki kwenye gari na kuitupa kwa madai ya kutotaka kurekodiwa na Paparazzi. Lakini Tukio hilo lilimpoza kwani Shabiki Yule aliripoti kwenye vyombo vya usalama na Jina la KANYE lilitajwa kama mshukiwa kwenye uchunguzi Wa Kesi Hiyo.


Share: