Jonathan majors akutwa na hatia za kumnyanyasa ex wake

Mahakama ya New york imemkuta na Hatia za unyanyasaji muigizaji wa movie za Marvel Jonathan Majors.

Major alikuwa na mashtaka mannne ya kumnyanyasa aliyekuwa mpenzi wake ( EX wake) Grace Jabbari,

Grace Aliiambia mahakama kuwa aliachwa na kidole kilichovunjika, michubuko, kukatwa nyuma ya sikio lake na maumivu "ya kupita kiasi".

Majors, 34, anakabiliwa na kifungo cha hadi mwaka mmoja jela, na amefukuzwa kutoka kwenye jukumu la kuigiza katika sinema zijazo za Marvel.

Share: