Jaivah amtaja oliver mtukudzi kwenye wimbo wake mpya wa 'story'

“Kipindi naandika hii ngoma nilikuwa namuona Oliver Mutukudzi. Yeye ndio aliyenifanya niandike na kufanya hii ngoma.” Amesema jaivah

Baada ya kufanya vizuri sana mwaka 2025 na ngoma ya Kautaka ambayo ilienda mpaka namba 1 kwenye chati mbalimbali za Nigeria, Jaivah amerudi tena na ngoma mpya ya kuitwa Story na Kwenye story Jaivah anabadilika kidogo. Kwenye wimbo huu Jaivah anakumbuka alipotoka ambapo anamuimbia kijana ambaye anaondoka kwenye nchi yake mama kwenda Johannesburg, Afrika Kusini. .

Kuhusiana na ngoma hii Jaivah amesema:

1.“Ngoma hii ni kama nimejishirikisha mwenyewe kwa sababu ukisikiliza hii nyimbo ni kama watu wawili tofauti wameimba humu ndani. Ukichukua verse ya kwanza na ya pili sauti ni tofauti japo ni mimi mimi ambaye nimeimba. Nadhani ni kitu ambacho sikuwahi fanya before na mashabiki zangu hopefully wataenjoy”

2. “Motivation ya wimbo huu, ni nimeongelea washkaji ambao wako mtaani. Mimi binafsi nimekulia mtaani eneo la Mburahati Dar Es Salaam. Kwa hiyo wimbo huu ni special kwa Wanangu wote wa Mburahati, Kigogo, Ilala na sehemu zote ambazo watu wana hustle.

Wimbo unamzungumzia mwana ambaye ali-hustle Tanzania baada ya kuona mambo magumu akatimkia South Africa”










Share: