J cole amuomba msamaha kendrick lamar

Rapper J cole amewashangaza mashabiki zake na wadau wa muziki wa rap Duniani baada ya kuomba msamaha jukwaani kwa kumdiss kendrick lamar siku za hivi karibuni

J Cole alifunguka kwenye Dreamville Fest ya kwamba na ifahamike kuwa yote ni mapenzi kati yake na Kendrick Lamar, kitendo hicho kimetafsiriwa kama udhaifu na wadau wengi wa hiphop.

kupitia mtandao wa X DJ Academics aliandika "J Cole kweli hakuwahi kujengwa kuwa namba 1 siku zote alikuwa mtoto wa Kati kiuhalisia amwachie Drake na Kendrick waendeleze battle."

hakuishia hapo aliendelea akaandika "Big 3 kuanzia sasa ni Drake, Kendrick Lamar na Future.

Uko upande upi kwenye Battle hili baina ya Kendrick Lamar na J Cole?!

Share: