India: halima kopwe anaongoza kwa kura nyingi miss world

Mrembo wa Tanzania, Halima Kopwe yupo nchini India akishiriki shindano la ulimbwende la dunia (Miss World), kupitia ukurasa wake wa Instagram @halimakopwe ametufahamisha kinachoendelea kwenye shindano hilo ambapo sasa anaongoza kwenye zoezi la upigaji kura kupitia website ya Miss World.

"Hadi sasa, tumeweza kushikilia namba moja kwa kura kwenye upande wa website visits. Ili kuniwezesha kubaki kileleni, tembelea website ya miss world iliopo kwenye bio yangu na kufuatilia matukio yangu mara kwa mara. Shindano la @missworld limeanza Februari 18 na fainali itafanyika Machi 09,2024.

Share: