Harmonize Atangaza mashindano ya kutafuta vipaji vipya nyanda za kusini mwa Tanzania

Staa wa Muziki wa Bongo Fleva Harmonize Ametangaza mashindano ya kusaka Vipaji aliyoyapa Jina la Konde Talent Search ambapo ataanzia Ruangwa na Mtwara.

Mbali na hivyo ameorodhesha majina ya Majaji watakao simamia zoezi Hilo ambao ni yeye mwenyewe, Masterj, Wema sepetu, Luludiva, Dj sevenworldwide, Kimambobeats na Bboybeats ambapo amesema.

"Kuelekea Tukaijaze Nangwanda !!! Ndugu zangu Wa Kusini Mwa Tananzania Kutana Na Hili Jukwaa Linaloweza Kubadili Maisha Yako Kama Kweli Una Kipaji Basi Wakati Wako Ndio Huuu !!!!! Ni Program Ya Siku 2️⃣ Kabla Ya Usiku Wa EID MOSI Mkoa Wa LINDI tunakutana RWANGWA tarehe 27 /3/ MTWARA MJINI tarehe 28 / Taratibu za Kujiandikisha Zitaanza Tarehe 25/3/ Ninaimani Kupitia Jukwaa Hili Tunaweza Kukutana Na Wakina KONDEBOY wengine !!! Fika Mapema Jiandikishe Pambania Kipaji Chako!!! Hakuna Gharama Yoyote Yakushiriki."


Share: