Mwanamitindo kutoka Tanzania, @hamisamobetto ametajwa kwenye orodha ya wanawake 10 duniani wenye wafuasi wengi zaidi kwenye Instagram, ambao ni wake au wapenzi wa wachezaji wa soka maarufu duniani (wanaojulikana kama WAGs – Wives and Girlfriends of footballers).

Katika ripoti mpya iliyotolewa na jarida la GMSSTATS_HP, Hamisa ametajwa kushika nafasi ya nane duniani, akiwa na zaidi ya wafuasi milioni 12.2 kwenye mtandao wa Instagram. Anatajwa kama Mke wa nyota wa Waydad na mchezaji wa kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki.