HADHARANI : MARIOO AMESHINDWA KUFICHA HISIA ZAKE AMUANDIKIA UJUMBE WA MAPENZI PAULA KAJALA

Msanii wa Bongo Fleva, Marioo, amemwandikia Paula Kajala ujumbe wa upendo kwenye siku yake ya kuzaliwa, akimtakia heri ya kutimiza miaka 23 na kueleza jinsi alivyo na thamani kubwa kwake.


Marioo aliandika:

"Heri ya kuzaliwa ya miaka 23 kwa mwanamke anayefanya maisha yawe na maana.

Sijui kama nitawahi kuwa na maneno sahihi kukuambia unavyonifanya nijisikie...

Lakini najua, kila nikikuangalia, naona kitu cha kipekee ambacho dunia haiwezi kunipa tena.

Wewe siyo tu mpenzi wangu, wewe ni sehemu yangu salama, sababu yangu, na uamuzi wangu bora zaidi.

Ukipotea, naumia. Ukicheka, dunia inatulizana. Ukiwa mbali, kuna kitu kinakosekana.

Nakuombea 23 iwe mwaka wako wa kung'aa hata zaidi, kufanikiwa, kupendwa... na mimi nikiwa karibu kushuhudia yote.

Nakupenda kwa njia ambayo hata moyo wangu mwenyewe haujaelewa kikamilifu.

Wewe ni wa milele kwangu. Na sitawahi kuacha kukuchagua."


Paula naye alijibu kwa kifupi akisema:

"ASANTE MY LOVE, NAKUPENDA SANA ❤️"


Wapenzi hao wameendelea kuonesha mahaba yao hadharani, wakivutia hisia za mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamii.

Share: