Flaviana matata anakuwa mwanamke wa kwanza tanzania kutajwa na forbes africa

Flaviana Matata ni Mwanamitindo na Mfanyabiashara muanzilishi wa Kampuni ya Lavy Products

Mwanamitindo Mtanzania Flaviana Matata amekua Mwanamke pekee kutoka Tanzania kutajwa kwenye orodha ya Jarida la FORBES AFRICA ya Wanawake hodari wa Afrika waliojitambua na kupata mafanikio kutokana na bidii yao ya kazi kwenye miongo yao isiyopungua mitatu.

Kwa mara kadhaa Jarida hili maarufu limekua likitangaza orodha za Wanawake hodari na wenye maono chini ya miaka 30 na zaidi ya miaka 50 lakini hii ni mara ya kwanza kutangaza orodha ya Wanawake hodari na wenye maono ambao umri wao ni miaka miaka 30 hadi 50.

Katika makala inayomuhusu Flaviana katika Jarida hilo la February/March 2024, kumeandikwa mengi lakini nanukuu haya machache aliyoyasema “wakiwa wanasimulia story yako ukiwa unatokea Afrika wanataka kuzungumzia upande wenye hadithi za umaskini tu ila mimi sina hiyo hadithi ya kuhuzunisha, ni kweli kuna umasikini Tanzania kama ilivyo kwenye Mataifa mengine ikiwemo Marekani japo haulingani lakini mimi sijatokea kwenye Familia masikini, Baba yangu alinipeleka kwenye Shule binafsi nzuri za Kanisa Katoliki”

“Wamagharibi huwa wanapenda kuonesha kwamba wewe ni Mtu unayetaka msaada wakati wote lakini nililikataa hilo toka mwanzoni, sijatokea kwenye Familia masikini, hata nilipoanzisha Kampuni yangu ya bidhaa za kucha Lavy Products walitaka kusema nimeileta bidhaa hiyo kwa ajili ya Wanawake wa rangi flani kitu ambacho sio kweli, nilianzisha Kampuni hii kwa ajili ya Mwanamke yeyote anayezipenda kucha zake, huwa wanapenda kukufungia kwenye box.mimi nilikataa”

Flaviana Matata ni Mwanamitindo na Mfanyabiashara muanzilishi wa Kampuni ya Lavy Products anayeishi na kufanya kazi New York Nchini Marekani na amefanya kazi na Makampuni mbalimbali kama Tommy Hilfiger, Vivienne na Westwood. 

Share: