Filamu ya Michael Jackson yakosolewa baada ya kuonekana ni yenye kumtetea

ilionyesha madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya Jackson na Wade Robson na James Safechuck kesi yao dhidi ya Jackson bado inasubiri kusikilizwa.

Filamu mpya ya MJ imeelezwa katika taarifa kadhaa za vyombo vya habari kama taswira ya uaminifu kuhusu maisha ya Michael Jackson, ikielekeza umakini kwa kipaji chake na mapambano yake ya kibinadamu. Lakini Graham King na John Logan, waandishi na waundaji wa filamu hiyo, wanaonyesha madai ya unyanyasaji kwenye filamu hiyo, kumbuka, Michael alipitia kesi ya jinai inayojulikana na watu wengi kuhusu madai hayo, lakini mwishowe wanamwonyesha kutokuwa na hatia kwa sababu hakupatikana na hatia wakati huo.

Katika taarifa tofauti, Graham King alisema hakusafisha maisha ya Michael hata kidogo, badala yake alifanya kazi kwa bidii kutoa taswira isiyopendelea upande wowote.

Lakini mkurugenzi wa "Leaving Neverland" Dan Reed haamini hilo, akiiambia kituo hicho kuwa amesoma nakala ya hati ya "Michael" na inaonekana kama ni wimbo wa sifa kwa MJ.

Kumbuka "Leaving Neverland" ilionyesha madai ya unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya Jackson na Wade Robson na James Safechuck kesi yao dhidi ya Jackson bado inasubiri kusikilizwa.

Reed anasema filamu hiyo inajitahidi sana kuonyesha Michael akishirikiana na watoto kwa njia chanya na hata anafika mbali kusema inaonekana kama wakili wa zamani wa Michael, John Branca mtayarishaji mtendaji kwenye filamu hiyo aliketi na timu ya ubunifu na kuwaambia moja kwa moja cha kuandika.

Share: