Dully sykes ametangaza ujio wa band yake mpya ya sykes music

Kuanzia kwenye ngoma zake hits kama ‘hi’ kupita hadi ‘dhahabu’ ya Kariakoo, kuibukia kwenye ‘baby candy’ hadi ‘hunifahamu’ na nyinginezo nyingi, sasa ni wakati wa kumfaidi mwenye Bongofleva yake katika muziki wa LIVE baada ya kutangaza rasmi leo kuja na Bendi yake ambayo atakuwa akitumbuiza nayo kwenye events mbalimbali atazoalikwa.

Staa wa Bongofleva Dully Sykes ametangaza rasmi kuja na Bendi yake iitwayo Sykes Music ambayo itaanza rasmi kazi June 1 2024 kwa kupokea mialiko ya kutumbuiza kwenye matukio mbalimbali kama vile harusi, sherehe za kiofisi na kwenye matukio mengine watakakoalikwa “tutakua tukiongea na Wateja watuambie wanahitaji mziki gani sio tu Bongofleva au nyimbo za Dully Sykes, hata wakitaka tupige miziki ya kikongo au kizungu au ya kiafrika tutafanya hivyo”

Hadi sasa Dully Sykes (43) ambaye ana miaka 25 tangu aingie rasmi kwenye muziki akiwa na nyimbo zaidi ya 200 alizozifanya mwenyewe pamoja na zile za kushirikishwa na Wasanii wengine, amesema Wateja wanaweza kuanza kufanya booking za Sykes Band kuanzia sasa kupitia namba 0713-45-96-60



Share: