Drake: hakuna mtu ambaye anaweza kugusa misingi yangu katika duniani hii

Ujumbe huu wa moja kwa moja ulijiri baada ya uvumi mkubwa kuhusu mgogoro unaomhusisha Drake na kundi la watu 15 walioungana dhidi yake

Mwimbaji maarufu wa Marekani, Drake, ametoa kauli rasmi kuhusu kundi la watu 15 walioungana dhidi yake, wakilenga kumkabili kwa namna moja au nyingine. Kupitia ujumbe wake wa hivi karibuni, Drake hakusita kuweka wazi msimamo wake.

"Amani, niko imara na kichwa changu kimeinuka juu, mgongo wangu umenyooka, nipo imara kabisa... na najua kwamba bila kujali nini, hakuna mtu mwingine ambaye anaweza kugusa misingi yangu katika duniani hii," alisema Drake kwa kujiamini.

Ujumbe huu wa moja kwa moja ulijiri baada ya uvumi mkubwa kuhusu mgogoro unaomhusisha Drake na kundi la watu 15 walioungana dhidi yake. Ingawa hakutaja moja kwa moja ni nani au ni kundi gani alilokuwa akizungumzia, maneno yake yalisisitiza ujasiri na kujiamini kwake mbele ya changamoto.

Drake, ambaye ni mmoja wa wasanii maarufu sana katika tasnia ya muziki ya Marekani, amekuwa akikumbana na vikwazo na upinzani katika kazi yake ya muziki, lakini bado ameweza kusimama imara na kufanikiwa kuvuka vikwazo hivyo.

Ujumbe wake unaonyesha azma yake ya kuendelea kusonga mbele na kufanikiwa licha ya changamoto zinazoweza kutokea. Mashabiki wake wamekuwa wakituma ujumbe wa kumtia moyo na kumshabikia katika kipindi hiki ambacho anaonekana kuwa katika majaribio.

Hadi sasa, hakuna taarifa zaidi kuhusu nini hasa kilichosababisha mgogoro huo au jinsi Drake anavyokusudia kushughulikia hali hiyo. Hata hivyo, kwa maneno yake, inaonekana kwamba yuko tayari kusimama kidete na kupigania mafanikio yake katika tasnia ya muziki. Mashabiki wake wanangoja kwa hamu kuona hatua zaidi za msanii huyo wa kimataifa.

Share: