dkt.mwinyi: Zanzibar kushirikiana na wasanii kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Wasanii kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii.


Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipokutana na Mwanamuziki kizazi kipya Omary Ally Mwanga maarufu Marioo , Ikulu Zanzibar tarehe 22 Julai 2024.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi amempongeza Marioo kwa kazi nzuri ya kuitangaza Tanzania kupitia kazi yake ya muziki.


Naye Marioo ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa fursa aliyoipata ya kurekodi wimbo wake mpya wa Hakuna Matata katika mazingira ya vivutio vya Zanzibar .

Pia amempongeza Rais Dkt.Mwinyi kwa jitihada zake kubwa za kuwaletea maendeleo wananchi wa Zanzibar.

Share: