Dj khaled kufanya kazi na tyler the creator

Dj maarufu kutoka Marekani DJKhaled amesema anatami kufanya kazi na rapa TylerTheCreator siku moja

Kwenye mahojiano na Rollingstone Khaled alisema “ningependa kufanya kazi na Tyler, nina maelewano nae mazuri licha ya mzozo ambao unaendelea kwenye mitandao ya kijamii”

Mvutano kati ya wawili hao ulionekana kushika kasi mwaka 2019 wakati Tyler aliposhinda tuzo yake ya pili ya Grammy, aliitumia ushindi huo kumtesa Khaled mtandaoni.

Kupitia Instagram Live, rapa huyo alisema “Asante DJ Khaled najua una hasira hakuna anayesikiliza albamu yako"

Share: