Diddy amefunguliwa kesi na mwanamitindo crystal mckinney anayedai alilazimishwa kushiriki ngono

Rapa na Mfanyabiashara Sean Combs “Diddy”, ameshutumiwa na Mwanamke aliyekuwa Mwanamitindo anayedai alilazimishwa kushiriki Ngono ya Mdomo bila ridhaa yake akiwa hajitambui

Crystal McKinney akiwa na umri wa miaka 22 alikutana na Diddy, Cipriani Downtown NYC Mwaka 2003 katika maonesho ya Mavazi ya Kiume, alipewa mwaliko kumtembelea rapa huyo katika Studio zake anakodai alifanyiwa Ukatili huo

Crystal amedai alimkuta Diddy akiwa na rafiki zake wakitumia Pombe na Kuvuta Vilevi ambapo alilazimishwa Ngono na alipokataa aligongeshwa Kichwa sakafuni kiasi cha kupoteza fahamu na kuja kuzinduka akiwa kwenye gari

Amedai alipata Msongo wa Mawazo na kutaka kujiua mwaka mmoja baadaye, hivyo amefungua Kesi ya kutaka kulipwa fidia ya Udhalilishaji huo. Ikumbukwe, Novemba 2023, Diddy alifunguliwa kesi pia na aliyekuwa mpenzi wake, Cassie Ventura lakini wakamalizana nje ya Mahakama. 

Share: