Diddy akumbwa na kesi ya ubakaji binti wa miaka 17

Mwanamke mwingine amejitokeza kumshutumu "Diddy" kwa ubakaji. Katika jalada la hivi punde, mwanamke aliyetambulika kama Jane Doe pekee anamshutumu mfanyabiashara mkubwa n pamoja na wanaune wa tatu kwa kumbaka alipokuwa na umri wa miaka 17.

Kesi ambayo iliwasilishwa Jumatano inasema kwamba tukio hilo linadaiwa kutokea ndani ya studio ya kurekodia ya Combs huko Manhattan mnamo 2003, Rolling Stone anaripoti. Kesi hiyo pia ilidai kuwa mwanafunzi huyo alisafirishwa kwa njia ya ndege na alipewa "kiasi kikubwa cha dawa za kulevya na pombe."

Share: