Diamond platnumz wenye thamani zaidi afrika

Mwanamuziki wa Tanzania, Diamond Platnumz, amevuka followers milioni 8.64 kwenye YouTube.

Anakuwa msanii wa kwanza na pekee wa Afrika kufikia hatua hii, huku mpinzani wake wa karibu kutoka Nigeria, Burna Boy akiwa na followers milioni 4.65.

Diamond Platnumz ni mmoja wa wasanii wenye thamani zaidi Afrika. Anatoza dola 100,000 kwa kila shoo la kimataifa pamoja na huduma ya ndege binafsi.

Mwenyeji lazima atoe na kumhudumia vinywaji, maji ya chupa 24 wakati wowote, taulo za uso 12, malazi bora na mengine mengi.

Kufikia mwaka 2024, thamani ya Diamond Platnumz inasimama kwa dola milioni 10, ikimweka kama mmoja wa wasanii tajiri zaidi Afrika.

Fally Ipupa wa DRC, anashika nafasi ya tatu na followers milioni 4.

Share: