
Msanii Diamond Platnumz afunguka na kuhusu video alizosambaza mwanadada Mange kimambi katika mitandao ya kijamii akiwa na mwanadada mrembo ajulikanaye kwa jina la Rita kuwa ni za zamani na walishaachana muda mrefu
Mapema usiku wa leo mwanamitandao Mange kimambi amevujisha video mbalimbali zikimuonesha msanii Diamond platnumz akiwa na mrembo mmoja anayejulikana kwa jina la Rita, wakiwa katika mahaba mazito na pia zikimuonesha mrembo huyo akiwa na ujauzito swala na ambalo limesumbua sana mitandaoni.
Diamond Platnumz ameamua kufunguka na kusema ukweli wote kuhusu video hizo ambapo amesema ni kweli alikuwa ni mpenzi wake mnamo mwaka 2023 ila kwasasa wameshaachana na hizo video ni za zamani na hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mtu aliyesambaza video hizo.