
A -List Artist Diamond Platnumz ametumia ukurasa wake wa Instagram kuwapa mashabiki wake ujumbe mzito kuhusu siri ya mafanikio yake kwenye sanaa.
Kupitia 'story' aliyoichapisha tena kutoka ukurasa wa #zongoclub, Diamond alionyesha umati mkubwa wa watu ukiburudika na wimbo wake, Komasava, huku akiambatanisha na maneno yanayoeleza kuwa mafanikio yake si ya kubahatisha..
Katika ujumbe huo, alieleza kuwa "Talent, Exposure, Mikakati, na Market Study" ndivyo vinavyofanya kazi zake ziwe kwenye "IQ nyingine kabisa."
Aliwaambia mashabiki wake kuwa anapotoa wimbo mpya, wao wanachopaswa kufanya ni kukaa na kufurahi kwa sababu anakuwa amefanya kazi kubwa kuhakikisha wimbo huo unawafikia wote..
Alimalizia kwa kusisitiza, "Nawafanya nyie proud... Trust me, sibahatishi, ninajua ninachokifanya," akionyesha jinsi anavyojiamini na kuwa na mikakati madhubuti katika kazi yake.