Davido kuchukua hatua za kisheria juu ya vyomba habari nchini kenya baada ya kuzusha kukamatwa uwanja wa ndege wa nairobi jkia

Nyota wa Afrobeats kutoka Nigeria, Davido, anasema anachukua hatua za kisheria dhidi ya shirika la vyombo vya habari nchini Kenya kuhusu hadithi ya Siku ya Wajinga ya Aprili ambayo ilikuwa "uzembe wa hali ya juu!."

Vyombo vya habari kwa kawaida huchapisha hadithi za utani za Siku ya Wajinga ya Aprili kuvutia umakini wa watu siku ya kwanza ya Aprili, lakini wakati mwingine pia zinaweza kwenda vibaya sana.

Davido hakufurahishwa kabisa wakati kituo cha K24 Digital linalomilikiwa na Mediamax Network Limited, lilipodai kuwa alikamatwa uwanja mkuu wa ndege wa Nairobi, JKIA, siku ya Jumapili baada ya upekuzi katika ndege yake binafsi.

K24 walisema nyota huyo wa Afrobeats na kikosi chake walikamatwa na kikosi cha polisi cha kupambana na dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta.

"Wakili wangu anatafuta njia za kisheria dhidi ya vyombo vya habari vinavyohusika kuzalisha taarifa hii potovu," Davido alisema, akiongeza kwamba hadithi feki hiyo ilisababisha "mfululizo wa masimu" kutoka kwa marafiki na jamaa walio na wasiwasi.

Share: