Davido asisitiza kuwa ameshaishinda afrika hivyo anaelekeza nguva zake marekani kimuziki

Mwanamuziki maarufu David Adeleke, anayejulikana kwa jina la Davido, amefichua nia yake ya kuuelekeza uangalifu wake kwenye ndoto yake ya Marekani, akisisitiza kuwa ameshashinda Afrika.

katika mahojiano na Billboard, alisema lengo lake ni kushirikiana na watu wenye vipaji kutoka duniani kote.

Davido aliongeza kwamba anafanya kazi kwenye albamu mbili, moja kwa Afrika na nyingine kwa Marekani.

Alisema: "Nataka kutoa albamu hii kwa idhini ya Mungu. Kwa matumaini, tutafanikiwa kufikia nafasi ya kwanza. Ninataka tu kushirikiana na wengine, kushawishi wengine, kuandika na kutengeneza muziki kwa ajili ya watu wengine. Ninafanya kazi kufikia ndoto. Ninaiishi ndoto yangu ya Kiafrika, sasa najaribu kufikia ndoto yangu ya Marekani."

Akizungumzia uhusiano wake na wasanii wa Marekani, Davido alisema: "Nadhani nina uhusiano mzuri na wasanii wa Atlanta, hasa baada ya kuishi huko kwa takriban miaka minne, mitano.

"Nina nyumba huko Atlanta, kwa hivyo linapokuja suala la utamaduni wa Marekani, nilijifunza mengi kusini.

"Kwa hivyo nadhani ninahusiana vizuri na wasanii wa Atlanta, nikiwa karibu na Young Thug na watu wengine. Kama vile, nilimfahamu Gunna hata kabla yangu au yeye kufanikiwa."

Davido alizaliwa Atlanta, Marekani lakini alihamia Nigeria akiwa mtoto mdogo.

Share: