Burna boy ku-perfom kwenye tuzo za grammy

Mwimbaji maarufu wa Nigeria burna boy atatumbuiza kwenye tuzo Kubwa za muziki duniani GRAMMYs za mwaka 2024 Jumapili, Februari 4 kwenye ukumbi wa Crypto.com huko Los Angeles, Marekani.

Grammy wametoa tarifa hiyo Januari 22, kwamba mwimbaji wa ‘City Boy’ Burna Boy, atashiriki katika jukwaa la Grammy na wasanii mashuhuri kama vile Luke Combs na Travis Scott. Na hii inamfanya burna boy kuwa msanii wa kwanza Africa kutumbuiza katika stage za Grammy

Share: