Billnass: wimbo wangu na diamond platnumz panatimka panatifuka na tunapindua juu chini

Rapper Billnass kwa sasa anaendelea na Promotion ya wimbo wake 'Number One' wimbo ambao amemshirikisha msanii Mbosso kutoka kwenye Record Label ya WCB Wasafi inayomilikiwa na Diamond Platnumz

Billnass ameweka wazi kuwa tayari amefanya wimbo na Diamond Platnumz ambapo anasubiri tu tarehe za kuachi project hiyo ambayo anasema ikitoka patatimka

"Wimbo wangu na Diamond ni wimbo mkubwa na mkali sana,naiamini muda wowote nikiachia najua panatimka panatifuka na tunapindua juu chini" alisema Billnass

Ungependa kuona kolabo ya wasanii hawa wawili Diamond na Billnass ikitoka lini?

Share: