BIG SEAN NA TUHUMA ZA UPASUAJI  KUTENGENEZA "6 PACKS "

Big Sean amevunja ukimya kuhusu uvumi uliosambaa mtandaoni kwamba tumbo lake limepata umbo zuri kwa msaada wa upasuaji au dawa za kuongeza nguvu.

Mnamo Julai 7, mshawishi wa mazoezi ya mwili, Blake Sanburg (@thenutritionnarc), alipakia video akidai kwamba misuli ya tumbo la rapa huyo inaonekana kama vile amepitia upasuaji au ametumia “steroids.” Sanburg alilinganisha picha za zamani za Big Sean na za sasa, akisema kuna mabadiliko makubwa, huku akitaja uwezekano wa kutumia mbinu ya “ab etching” (upasuaji wa plastiki unaochonga misuli ya tumbo), lakini pia akakiri kwamba Sean anaweza kuwa na “genetics nzuri” za asili.


Baada ya video hiyo kusambaa, Big Sean alijibu moja kwa moja kwenye sehemu ya maoni, akisema“Bro, unfortunately mine are real lol”, akimaanisha kwamba misuli yake ni ya asili kabisa. Aliongeza kuwa kila mtu ana mwili tofauti na hata alitania kwamba akiacha mazoezi anaonekana kama “chewed up tootsie roll” (yaani anaonekana ovyo).

Sanburg baadaye alifichua kuwa Big Sean pia alimtumia ujumbe binafsi, ambapo Sean aliandika,“Niliongeza uzito wa ubaba na nikalazimika kurudi mazoezini kwa bidii kadri nilivyozidi kuzeeka bro. Kwa hiyo mwili wangu umepitia mengi lol. Lakini hakuna upasuaji.”


Big Sean kwa muda mrefu amekuwa akizungumzia kuhusu kujitolea kwake kwa mazoezi ya mwili, hasa baada ya kuwa baba. Katika mahojiano ya hivi karibuni na Jay Shetty kwenye podcast ya On Purpose, alielezea pia kuhusu jinsi alivyokabiliana na msiba wa kupoteza wapendwa wake, akihamasisha watu kushughulikia huzuni bila kuiacha iwaangushe.

Share: