Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesitisha shughuli za Sanaa kwa kumbi za starehe 504

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesitisha shughuli za Sanaa, Starehe na Burudani katika Kumbi 504 za Tanzania Bara kutokana na kutotimiza vigezo baada ya kuhuisha vibali kuanzia Machi 28, 2024 mpaka watakapolipia vibali kupitia Mfumo wa AMIS. 

BASATA imesema imefikia hatua hiyo baada ya Wamiliki wa Kumbi 149 kutimiza maelekezo ya usajili kati ya 653 waliyopewa maelekezo ya kufanya hivyo awali mnamo Februari 19, 2024 ambapo walipewa Siku 14 wakamilishe mchakato huo. 

Baadhi ya Kumbi hizo ni Bilicanas Club (Arusha), Fuego Lounge, Dar Live, Lango la Jiji, Dar West Inn na Lamada Hotel. 

Share: