Treni mchongoko haijapata hitilafu, taarifa zilikuwa za uzushi

hirika la Reli Tanzania (TRC) limetaka kupuuzwa kwa taarifa zinazosambazwa na baadhi ya watu kuhusu kusimama kwa treni mpya za kisasa 'mchongoko' huku wakihusisha jambo hilo na changamoto za umeme.

Katika taarifa yake TRC imesema tangu kuanza kwa safari ya kwanza ya treni zinazotumia nishati ya umeme Juni 14, 2024 hakujawahi kuwa na changamoto ya umeme.

imesema kilichotokea Novemba 03, 2024 na kusababisha kusimama kwa treni ya mchongoko kwa takribani saa sita ni hujuma kutokana na kukatika ama kukatwa kwa nyaya zinazochukua umeme kutoka njia ya umeme kupeleka kwenye treni.

Shirika la Reli Tanzania limeuhakikishia umma kuwa hakuna treni ya mchongoko iliyopata hitilafu ya kiufundi.

Tayari baadhi ya wahusika wamekamatwa na hatua stahiki dhidi yao zimeshaanza kuchukuliwa ikiwemo kufikishwa kwenye vyombo husika.

Share: