Tiktok imefungua kesi inayolenga kuzuia sheria ya marekani ambayo itapiga marufuku programu hiyo ya video nchini humo

TikTok imefungua kesi inayolenga kuzuia sheria ya Marekani ambayo itapiga marufuku programu hiyo ya video nchini humo labda iuzwe.

Katika jalada hilo, kampuni hiyo ya mitandao ya kijamii imesema kitendo hicho ni "uingiliaji wa ajabu wa haki za uhuru wa kujieleza" wa kampuni hiyo na watumiaji wake milioni 170 wa Marekani.

Ilisema Marekani ilikuwa imezua "wasiwasi wa kukisia" tu ili kuhalalisha hatua hiyo na ikaomba mahakama isimamishe.

Rais Joe Biden alitia saini mswada huo kuwa sheria mwezi uliopita, akitoa sababu za usalama wa taifa.

Hatua hiyo ilifuatia mjadala wa miaka mingi huko Washington, ambayo imedai kuwa umiliki wa TikTok wa Uchina huongeza hatari kwamba data ya watumiaji raia wa Marekani inaweza kuangukia mikononi mwa serikali ya Uchina au kutumika kwa propaganda.

Hata hivyo, TikTok imeshikilia kuwa inajitegemea, huku kampuni mama ya ByteDance ikisema haina mpango wa kuuza biashara hiyo.

Serikali ya Uchina imekosoa sheria hiyo kama "uonevu" wa Marekani kwa kampuni ya kigeni na kuashiria kuwa ingepinga uuzaji.

Share: