Tigo tanzania imekabidhiwa rasmi tuzo ya mtandao wenye kasi zaidi

Kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania hatimaye imekabidhiwa rasmi Tuzo iliyoshinda baada ya kutajwa kuwa Mtandao wenye kasi zaidi Tanzania kwa mwaka 2023 iliyotolewa na Taasisi ya Kimataifa ya Ookla yenye Makao yake makuu Washington Seattle Nchini Marekani.

Taarifa ya Tigo kwa Vyombo vya habari imesema Tuzo hii imetokana na matunda ya uwekezeji unaoendelea kufanywa na Kampuni hiyo kote Tanzania katika kuboresha miundombinu ya mtandao wake tangu miaka takribani miwili iliyopita.

Itakumbukwa kwamba mwaka 2022 Tigo Tanzania ilitangaza rasmi kuanza kutekeleza mpango wake wa miaka mitano unaolenga kuwekeza kiasi cha shilingi za kitanzania zaidi ya Trilioni moja za kitanzania kwenye kuboresha miundombinu ya mtandao wake ambapo uwekezaji huu ni moja kati ya vipaumbele vya kampuni ya Axian Telecom Group ambayo haina muda mrefu toka iinunue Kampuni ya Tigo Tanzania.

Ookla ni Taasisi ya kimataifa iliyoanzishwa mwaka 2006 ambapo moja kati kazi inazofanya ni kupima kiwango cha ubora wa huduma za intaneti duniani ikiwemo ‘speed test’ au kipimo cha kasi ya intaneti pamoja na uharaka kupakua au kupakia maudhui mtandaoni.

Share: