Nape amesema kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na TCRA hivi karibuni kuna ongezeko kubwa la laini ukilinganisha na mwaka 2002
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Nape Nnauye amesema Sekta ya Mawasiliano Nchini inazidi kukua kwa kasi ambapo mpaka sasa kuna jumla ya laini za simu zinazofanya kazi ‘active’ milioni 72.
Waziri Nape ameyasema hayo leo April 25,2024 Jijini Dodoma mbele ya Makamu wa Rais wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango katika Hafla ya Uzinduzi wa Jengo la Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote.
Nape amesema kwa mujibu wa Takwimu zilizotolewa na TCRA hivi karibuni kuna ongezeko kubwa la laini ukilinganisha na mwaka 2002 ambapo kulikuwa na jumla ya line za simu milioni 51.
“Mwaka 2002 kulikuwa na jumla ya laini za simu milioni 51, takwimu mpya zilizotolewa mwaka huu na TCRA zimeonesha tuna laini za simu zilizo active Milioni 72, ambapo pia jumla ya line milioni 32 zimeunganishwa na huduma za kifedha ikiwa ni ongezeko kubwa ukilinganisha na mwaka 2020 ambapo jumla ya laini za simu milioni 5 pekee zilikuwa zimeunganishwa na huduma za kifedha”