Sua yatoa mafunzo ya mfumo akili bandia

Mafunzo hayo ya Mradi wa kutengeneza mfumo huo una matarajio kuasaidia kufuatilia, kutabiri na kupendekeza njia bora za kukabiliana na magonjwa yanayosumbua mimea.

Chuo kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA), kimetoa Mafunzo ya mfumo wa akili bandia kwa afya ya mimea kwa baadhi ya wakulima wa Wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani yenye lengo la kusaidia kufuatilia njia bora za kukabiliana na magonjwa ya mimea.

Mafunzo hayo ya Mradi wa kutengeneza mfumo huo una matarajio kuasaidia kufuatilia, kutabiri na kupendekeza njia bora za kukabiliana na magonjwa yanayosumbua mimea.

Dkt. Michael Mahenge kutoka SUA amesema mradi huo unafanywa kwa kushirikiana na mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali ambayo ni shirika linalokabiliana na viumbe viharibifu (TPHPA) na (RECODA) shirika linalojishughulisha na kuweka daraja la Teknolojia ili ziweze kuwafikia wakulima hasa wale wadogo kwa urahisi itakayowezesha kuendelea sehemu mbalimbali kwa kilimo chenye tija kwa kutumia mfumo wa jitihada shirikishi za kuleta mageuzi ya kilimo vijijini.

Share: