Serikali ya Marekani inatumai wakifanikisha hilo litasaidia kudumisha juhudi za kitaifa na za kibinafsi za kufikia mwezi.
Wanasaikolojia wa Marekani huenda hivi karibuni wakagundua jambo, kwani Ikulu inataka Mwezi uwe na muda wake (time zone).
Shirika la anga la Marekani, Nasa, limeombwa kuendeleza (develope) muda wa mwezi, utakao itwa Coordinated Lunar Time (CLT).
Serikali ya Marekani inatumai wakifanikisha hilo litasaidia kudumisha juhudi za kitaifa na za kibinafsi za kufikia mwezi.
"Saa ya atomiki kwenye Mwezi itatikisa kwa kiwango tofauti na saa kwenye Dunia," alisema Kevin Coggins, afisa mkuu wa mawasiliano na urambazaji wa Nasa.
"Inaelekea kwamba unapokwenda nje ya Dunia, kama Mwezini au kwenye sayari ya Mars, kila sehemu ina mapigo yake tofauti ya moyo" aliongeza.