mafundi wanofanyakazi katika kiwanda hicho wengi wao wamesoma chuo cha usafirishaji (NIT)
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Profesa Godius Kahyrara amesema kuwa wizara yake inategema kukutana na Wizara ya Fedha ili kuweka utaratibu wa kusidia sekta ya Anga hasa kwa kampuni zinazounganisha na kutengeneza ndege hapa nchini.
Kahyrara amesema hayo baada ya kutembelea Kampuni ya Airplane Africa Limited iliyopo Mazimbu mkoani Morogoro inayomilikiwa na wawekezaji kutoka jamhuri ya Czech ambayo inafanya kazi ya kuunganisha na kutengeneza ndege za kubeba abiria wawili mpaka wanne.
Kahyrara ameongezea kuwa mafundi wanofanyakazi katika kiwanda hicho wengi wao wamesoma chuo cha usafirishaji (NIT) hivyo ni muhimu kwa kiwanda hicho kwani kitasaidia kutoa uzowefu kwa wanafunzi wa kutoka vyuo vya Vikuu, , vyuo vya kati na Vyuo vya Ufundi.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda hicho Mhandisi Igor Stratl amesema kuwa wamevutiwa kuwekeza Tanznia kwasababu ni nchi yenye Usalama, Utulivu na Amani hivyo imewarahisishia kufanya kazi zao muda wote. Kiwanda hicho kilichoanza mwaka 2021 mpaka sasa kimeunganisha na kutengeza ndege zaidi ya tatu na ndege hizo zinaweza kuuzwa katika nchi mbalimbali.