Open AI yaungana na Kakao kuimarisha upanuzi wa AI
Kampuni ya Marekani ya teknolojia ya akili bandia (AI), #OpenAI, imetangaza kuingia ubia na kampuni kubwa ya teknolojia ya Korea Kusini, #Kakao, ili kuimarisha upanuzi wake katika ukanda huo. Afisa Mtendaji Mkuu wa OpenAI, Sam, alitangaza ushirikiano huo kwenye sherehe iliyofanyika Seoul pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kakao, Chung Shin-a. Ushirikiano huu unalenga kuunda bidhaa ya AI iliyoboreshwa kwa soko la Korea Kusini.
Katika hatua nyingine, OpenAI na #SoftBank ya Japan wameanzisha kampuni ya pamoja inayoitwa SB OpenAI Japan, huku SoftBank ikipanga kutumia karibu euro bilioni 3 kila mwaka kuingiza huduma yake ya AI, Cristal, katika kampuni zake kama Arm na #PayPay. Cristal itatumika kusaidia kampuni katika upangaji, masoko, na hata kuchambua vyanzo vya zamani vya programu.
Mradi wa #Stargate, unaoungwa mkono na Rais #DonaldTrump, pia umepangwa kupanuka hadi Japan na nchi nyingine. Stargate inalenga kuwekeza hadi dola bilioni 500 katika miundombinu ya AI nchini Marekani, kwa ushirikiano na #Oracle.