Mwanajeshi wa zamani wa marekani afanyiwa upasuaji wa kwanza duniani wa kupandikizwa jicho

Madaktari wa upasuaji mjini New York wanasema kuwa wamefanya upasuaji wa kwanza duniani wa kupandikiza jicho kamili kwa mwanamume, ingawa hakuna uhakika kuwa ataweza kuona tena.

Aaron James, ambaye alinusurika kwenye ajali ya umeme , alifanyiwa upasuaji wa saa 21 ambao ulibadilisha nusu ya uso wake.

Madaktari wa upasuaji wameweza kupandikiza konea kwa mafanikio kwa miaka.

Wataalamu wameita mafanikio hayo kuwa muhimu katika azma ya kuwawezesha mamilioni ya watu kuona.

Bwana James, mfanyakazi wa laini ya umeme kutoka Arkansas, alipoteza sehemu kubwa ya uso wake wakati ilipogusa kwa bahati mbaya waya wa moja kwa moja wa volti 7,200 mnamo 2021.

Mnamo tarehe 27 Mei mwaka huu, alifanyiwa upandikizaji wa nadra wa sehemu ya uso pamoja na upandikizaji wa macho - ambao ulihusisha zaidi ya wataalamu 140 wa afya.

Madaktari wa upasuaji katika NYU Langone Health, ambao walifanya upasuaji huo mgumu, walisema Alhamisi kwamba Bw James, 46, alikuwa akipata nafuu baada ya kupandikizwa mara mbili na jicho lililotolewa lilionekana kuwa na afya tele.Jicho lake la kulia bado linafanya kazi.

Share: