Mtambo wa kutibu magonjwa zaidi ya 10 wazinduliwa muhimbili

Hospitali ya Taifa Muhimbili imezindua mtambo unaotumia hewa tiba yenye mgandamizo ya oksijeni (Hyperbaric Medicine Treatment) ambao unatibu magonjwa zaidi ya 10 na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na  ya pili Kusini mwa Jangwa la Sahara kutumia mtambao huo uliogharimu TZS. 250  Mil.

 Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa mtambo huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Prof. Mohamed Janabi amesema kupitia matibabu haya mgonjwa huingizwa kwenye kifaa maalumu na kupatiwa tiba kupitia hewa tiba ya oksijeni iliyogandamizwa kwa 100%.

 Ameyataja wagonjwa watakaonufaika kuwa ni wale wenye vidonda sugu ambavyo matibabu mengine yameshindikana kama wagonjwa wa sukari, walioathirika na moshi baada ya kuungua na moto na waliopata changamoto za upungufu wa oksijeni mwilini kama waliozama kwenye maji baharini n.k.

 Ameongeza kuwa wagonjwa wengine waliopata mionzi na kusababisha sehemu zilizopata tiba mionzi kuathitika ikiwemo wenye saratani za koo, njia ya chakula na wale wenye tezi dume,waliofanyiwa upasuaji na kuwekewa/kupandikiziwa sehemu ya miili yao, wenye changamoto ya kusikia,wenye tatizo la usaha kwenye ubongo, wenye changamoto ya oksijeni kwenye mishipa ya damu (arterial insufficiencies) na watoto wenye usonji.

 Prof. Janabi ameishukuru Kampuni ya Sechrist ya nchini Marekani ambao ndio watengenezaji na ndiyo waliotoa msaada huo wenye thamani ya TZS. 250 Mil.

 Amemshukuru Jaclyn Mackey pamoja na uongozi mzima wa Woundcare Education Partners, John Peters ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa Undersea and Hyperbaric Medical Society ambao kwa nyakati tofauti waliweza kutoa nafasi za mafunzo na kuwaidhinisha madaktari watatu (Certified Hyperbaric Physician) pamoja na wauguzi watano (Certified Hyperbaric Nurses) ambao wataendelea kutumia mtambo huo kuhudumia wananchi.

 Aidha, Prof. Janabi amemshukuru na Prof. Jay Buckley ambaye kupitia ushirikiano wake wa kitabibu na kitafiti kati ya Chuo Kikuu anachofanya kazi cha Dartmouth nchini Marekani na MUHAS alifanikisha upatikanaji wa mtambo huu.

Katibu Mkuu UWT (T) Komredi Jokate Mwegelo amepokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Songea Mkoani Ruvuma na Komredi Odo Mwisho Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro Waziri wa Michezo na Mbunge wa Songea Mjini, Komredi Kuruthumu muhagama Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Ruvuma pamoja na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali.

Share: