Hali hiyo imesababisha kiasi cha Bidhaa 287 zilizoagizwa kuwa zaidi ya mahitaji halisi
Ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika mifumo ya TEHAMA kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 inaeleza Mfumo wa Epicor katika Bohari ya Dawa (MSD) una upungufu katika kulinganisha kiasi cha andiko la manunuzi dhidi ya mahitaji halisi
Hali hiyo imesababisha kiasi cha Bidhaa 287 zilizoagizwa kuwa zaidi ya mahitaji halisi, na bidhaa 3,137 zilizoagizwa na kufadhiliwa na MSD kutokuwa na mahitaji linganifu
CAG ameeleza upungufu huo unaweza kusababisha Ubadhirifu, kama vile kuunda Mikataba ya manunuzi ambayo haikuidhinishwa au kupandisha gharama na hivyo kusababisha hasara za kifedha.
Share: